KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 17, 2010

ALMUNIA NI BORA KULIKO !!!!!


Wakati Liverpool wakijiandaa kumpokea kipa mpya, ushauri wa bure umetolewa kwa washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal walio kwenye harakati za kusaka kipa mwingine katika kipindi hiki cha usajili.

Ushauri huo wa bure umetolewa na nahodha wa zamani wa kikosi cha Arsenal Stewart Robson ambaa amesema Manuel Almunia ni kipa mzuri kuliko makipa wanaofikiriwa kusajiliwa klabuni hapo Mark Schwarzer ama Shay Given.

Robson aliyeitumikia Arsenal toka mwaka 1981-86 amesema Almunia hana tatizo lolote kama inavyofikiriwa na wengi na hakuwahi kumsikia mtu yoyote akisema Mark Schwarzer ama Shay Given ni bora kuliko kipa huyo wa kimataifa toka nchini Hispania.

No comments:

Post a Comment