KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 26, 2010

ANAEKOSA NI WAJIBU AADHIBIWE !!!


Meneja wa klabu ya Stoke City Tony Pulis ameahidi kumchukulia hatua za kinidhamu kipa wake nambari mbili Asmir Begovic kufuatia kukataa kucheza mchezo wa kuwania ubingwa wa kombe la ligi uliochezwa usiku wa kuamkia jana dhidi ya Shrewsbury waliokubali kisago cha mabao mawili kwa moja.

Tony Pulis amesema kitebndo cha kipa huyo kukataa kucheza mchezo huo bado kinamkera na atahakikisha suala hilo analifikisha katika kamati ya nidhamu ili hatua hizo za kinidhamu zichukue mkoando wake.

Amesema kipa huyo wa kimataifa toka nchini Bosnia anatakiwa kuwa na nidhamu wakati wote klabuni hapo na kama atakwenda kinyume na hatua hiyo anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Hata hivyo tayari imeshaelezwa kwamba kugoma kwa kipa huyo kumetokana na kutaka kuushinikiza uongozi wa klabu hiyo kumuuza katika klabu ya Chelsea yenye lengo la kumsajili.

No comments:

Post a Comment