KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 19, 2010

ANDERSON KUREJEA UWANJANI.


Baada ya kuwa nje kwa kipindi cha miezi sita iliyopita kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil na klabu ya Manchester United Anderson Luís de Abreu Oliveira yu njiani kurejea katika hali yake ya kawaida.

Anderson Luís de Abreu Oliveira amezungumza na vyombo vya habari akiwa nchini Ureno alipo kwa sasa akipatiwa matibabu ya goti lake amesema anaendelea vyema na anajisikia vizuri.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 amesema kujisikia kwake vizuri kunampa nafasi ya kujiona yupo karibuni kurejea uwanjani kuisaidia klabu yake iliyopania kurejesha heshima huko Old Trafford.

No comments:

Post a Comment