KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 17, 2010

ANELKA APEWA ADHABU.



Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Nicolas Anelka hatoruhisiwa kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa michezo 18, baada ya Shirikisho la soka nchini Ufaransa kutoa tamko kama adhabu kwa mchezaji huyo.

Adhabu hiyo kwa Anelka imetangazwa hii leo, baada ya mitafaruku kujitokeza kati yake na aliekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Raymond Domenech walipokua kwenye fainali za kombe la dunia huko nchini Afrika kusini.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini Ufaransa imeeleza kuwa mshambuliaji huyo ataruhusiwa kurejea katika timu ya taifa endapo akitaka kufanya hivyo baada ya michezo 18 kupita.

Hata hivyo huenda adhabu hiyo ikawa kazi bure kwa mshambuliaji huyo, kwani kama itakumbukwa vyema mara baada ya kurejea jijini London akitokea Afrika kusini baada ya kufukuzwa kwenye kikosi alitangaza kustahafu soka la kimataifa.

Mbali na Nicolas Anelka kupewa adhabu hiyo, aliekua nahodha wa kikosi cha Ufaransa kwenye fainali za kombe al dunia Patrice Evra, nae ameadhibiwa kutokucheza michezo mitano ya timu ya taifa baada ya kuthibitika alionyesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kocha wa viungo walipokua bondeni Afrika kusini.

No comments:

Post a Comment