KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Sunday, August 15, 2010

ARSENAL YAGOMA KUPOTEZA POINT.Baada ya matokeo ya sare ya bao moja kwa moja, meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson amekiri kusikitishwa na matokeo hayo yaliyopatikana mbele ya washila bunduki wa Ashburton Grove Arsenal.

Roy Hodgson amesema tayari kikosi chake kilikua na sababu zote za kumaliza pambano hilo la jana kwa ushindi na kuibuka na point tatu muhimu lakini makosa yalioyofanywa na kipa wake wa kimataifa toka nchini Hispania Pepe Reina yamewagharimu na kujikuta wakizipoteza point mbili.

Nae meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema wachezaji wake walionyesha uchu wa kufuta makosa yaliyojitokeza mwanzoni mwa kipindi cha pili yalioyopele kuwapa bao la kuongoza Liverpool, kwa kucheza vyema na kulishambulia lango la wapinzani wao.

Amesema kwa uhalisia huo wachezaji wake walistahili kupata ushindi lakini matokeo yaliyopatikana yamekua afadhali kwa Liverpool ambao kwa kipindi chote walikuwa wakizuia.

Katika mchezo huo kiungo mpya wa klabu ya Liverpool Joe Cole alionyesjhwa kadi nyekundu katika dakika ya 45 baada ya kumchezea rafu mbaya beki mpya wa klabu ya Arsenal Laurent Koscielny ambae nae alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 90 baada ya kuunawa mpira.

No comments:

Post a Comment