KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 19, 2010

ARSENAL YATUMA OFA SEVILLA.


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger yu mbioni kukamilisha ahadi aliyoitoa kwa mashabiki wa klabu hiyo ya kumsajili beki mmoja ama wawili katika pindi hiki cha usajili kilichosalia.

Wenger yu mbioni kukamilisha suala hilo baada ya kutuma ofa kwenye klabu ya Sevilla ya nchini Hispania ya kutaka kumsajili beki wa kimataifa toka nchini Ufaransa Sebastien Squillaci.

Ramon Rodriguez mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Sevilla hii leo amezungumza na vyombo vya habari akiwa uwanja wa ndege wa mjini Porto huko nchini Ureno walipokua wakicheza mchezo wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya FC Bragha na kuthibitisha ni kweli wamepokea ofa hiyo toka Arsenal.

Ramon Rodriguez amesema baada ya kupokelewa kwa ofa hiyo kinachofuata ni mazungumzo ya kuuzwa kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 30 ambae tayari ameshaichezea Sevilla michezo 49 na kufunga bao moja.

Arsene Wenger anatarajia kumsajili S├ębastien Squillaci baada ya kuondoka kwa Sol Campbell, William Gallas pamoja na Mikael Silvestre ambao wote klwa pamoja mikataba yao ilifikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment