KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Sunday, August 22, 2010

BADO NIPO NIPO SANA.


Beki wa kimataifa toka nchini Norway na klabu ya Fulham ya nchini Uingereza Brede Hangeland amekanusha taarifa za uvumu zinazomuanda kwa sasa juu ya kutaka kuihama klabu yake na kujiunga na klabu ya Arsenal ama Liverpool.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 amesema taarifa hizo kila leo zimekua zikimuanda na ila ifahamike hazina ukweli wowote na yeye daima ataendelea kusalia huko Croven Cottege yalipo makao makuu ya klabu yake ya sasa Fulham Fc.

Amesema kuhusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu kadhaa za nchini Uingereza ama nje ya nchi hiyo ni kitu cha kawaida hivyo haoni ajabu katika hatua hiyo lakini yeye binafsi anatambua bado ni mchezaji halali wa The Cottagers.

Brede Hangeland amelezimika kulitolea ufafanuazi suala hili, baada ya kufuatwa na vyombo vya habari kwa kipindi cha majuma mawili sasa huku vikitaka kujua ukweli wa suala hilo.

Hata hivyo ameongeza kwamba bado ni mwenye furaha huko Croven Cottege na hafikirii kuondoka kwa sasa licha ya kuzungumzwa sana juu ya kutaka kujiunga na klabu ya Arsenal pamoja na Liverpool zinazohaha kuimarisha vikosi vyao kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili mwishoni mwa mwezi huu.

Hii si mara ya kwanza kwa beki huyo kuhusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu ya Arsenal na mara kadhaa klabu hiyo ya London kila inapotuma ofa ya kumsajili imekua ikikataliwa.

Brede Hangeland alisajiliwa na klabu ya Fulham mwaka 2008 akitokea nchini Denmark katika klabu ya F.C. Copenhagen na mkataba wake na The Cottagers unatarajia kufikia kikomo mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment