Klabu ya Manchester United imekamilisha usajili wamshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ureno na klabu ya Vitoria de Guimaraes - Tiago Manuel Dias Correia Bebe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na uongzoi wa klabu hiyo ya jijini Manchester zimeeleza kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amesajiliwa baada ya kupita kwenye vipimo vya afya alivyofanyiwa siku mbili zilizopita.
Mshambuliaji huyo mwenye urefu wa futi 6 na nchi 3 amejiunga na klabu hiyo na mashetani wekundu kwa ada ya uhamisho wa paund million 7.4.
Kusajiliwa kwa Tiago Manuel Dias Correia Bebe kunaifanya klabu ya Man utd kufikisha idadi ya wachezaji watatu waliosajiliwa katika kipindi hiki ambapo mjiongoni mwa wachezaji hao ni Javier Hernandez Chacharito toka nchini Mexico pamoja na Christopher Lloyd Smalling.
No comments:
Post a Comment