KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 16, 2010

BELLAMY KUJIUNGA NA CARDIFF CITY?


Baada ya kuachwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 cha klabu ya Man City, winga wa kimataifa toka nchini Wales Craig Bellamy anakaribia kujiunga na klabu ya Cardiff City inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza.

Cardiff City waliomaliza katika nafasi nne za juu msimu uliopita wameripotiwa kukaribia kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 31, baada ya meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini kuridhia kuondoka kwake.

Msemaji wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu huko Cardiff City Stadium amesema licha ya wao kuwa katika utaratibu wa kumsajili Bellamy pia kuna baadhi ya vilabu vimeonyesha nia kama hivyo lakini muhusika yu tayari kujiunga nao.

No comments:

Post a Comment