KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 25, 2010

BRADLEY AYATAMANI MAISHA YA UINGEREZA.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani Bob Bradley hatimae amepasua ukweli wa kuifukuzia kazi ya umeneja wa klabu ya Aston Villa ambayo bado ipo chini ya meneja msaidizi Kevin MacDonald.

Akizungumza kwa njia ya simu toka nchini kwao Marekani Bob Bradley amesema anapenda sana kufanya kazi nchini Uingereza na amanini iupo siku suala hilo litatimia.

Hata hivyo meneja huyo amedai kuwa bado hajafuatwa kuombwa kufanya kazi nchini Uingereza hususana katika klabu anayohusishwa nayo kila kukicha lakini upo uwezekano mkubwa wa suala hilo likajitokeza.

Bradley alianza kuhusishwa na taarifa za kujiunga na klabu ya Aston villa mara baada ya kuondoka kwa Martin O’Neil mwanzoni mwa mwezi huu huku sababu ikielezwa ni mvurugano uliojitokeza kati ya meneja huyo dhidi ya bosi wake.

No comments:

Post a Comment