KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 24, 2010

CAMEROON KAMA UFARANSA !!!!!!


Kocha mpya wa timu ya taifa ya Cameroon Javier Clemente Lázaro amewatema wachezaji wa timu hiyo walioonekana kuwa tatizo kwenye kikosi kilichoshiriki fainali za kombe la dunai huko nchini Afrika kusini mwaka huu.

Javier Clemente Lázaro kocha wa kimataifa toka nhini Hispania amewatema wachezaji hao huku akiwachukua baadhi ya wachezaji waliokuwepo katika kikosi kichoshiriki fainali za kombe la dunia sambamba na wachezaji walioitwa katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Poland majuma mawili yaliyopita.

Miongoni mwa wachezaji walioachwa kwa sababu za kuonekana ni tatizo ni Alexandre Song Bilong, Achille Emana pamoja na Carlos Idriss Kameni huku Rigobert Song akijumuishwa katika kundi hilo licha ya kutangaza kustahafu soka la kimataifa.

Akilitolea ufafanuzi suala hilo kocha msaidizi wa kikosi cha Cameroon kinachojiandaa na mchezo wa kundi la tano wa kuwani nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya afrika mwaka 2012 dhidi ya Mauritania Francois Omam Biyick amesema bosi wake Javier Clemente Lázaro ameona ni bora kuanza na wachezaji wenye muelekeo wa kulisaidia taifa la Cameroon.

Hata hivyo Francois Omam Biyick amesema kuachwa kwa wachezaji hao hakumaanishi hawatoitwa tena kikosini bali wataitwa kutokana na umuhimu wao utakapohitajika.

No comments:

Post a Comment