KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 26, 2010

CARLOS ARNOLDO SALCIDO FLORES ANUSA LONDON.


Meneja wa klabu ya Fulham Mark Hughes yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa klabu ya PSV Eindhoven ya nchini uholanzi Carlos Arnoldo Salcido Flores.

Hughes anatarajia kumaliza usajili wa beki huyo wa kimataifa toka nchini Mexico kufuatia mazungumzo kati ya vilabu hivyo viwili kwenda sawa bin sawia.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 30, ambae pai alikua anawaniwa na klabu ya Liverpool, yu njiani kuelekea nchini Uingereza huku ada yake ya uhamisho ikitajwa kuwa ni paund million £1.6.

Hata hivyo imeelezwa kusajiliwa kwa Carlos Arnoldo Salcido Flores, kunafuatia hatua ya beki wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Fulham Paul Konchesky kuwa na uwezekano wa kujiunga na meneja wake wa zamani Roy Hodgson aliejiunga na klabu ya Liverpool mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Mapema hii leo meneja wa klabu ya Fulham Mark Hughes alitangaza kuwa na matumaini ya kumsajili Carlos Arnoldo Salcido Flores kwa lengo la kutoa nafasi kwa Paul Konchesky kutimiza ndoto zake za kuelekea Anfield.

Kukamilika kwa usajili wa beki huyo wa kushoto kutaifanya klabu ya Fulham kufikisha idadi ya wachezaji watatu waliowasajili katika kipindi hiki ambao ni Rafik Halliche, Mousa Ndembele pamoja na Carlos Arnoldo Salcido Flores.

No comments:

Post a Comment