KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 13, 2010

CHELSEA MDOMONI MWA FIFA !!.


Uongozi wa klabu ya Santos umepanga kuishitaki klabu ya Chelsea katika ngazi za juu za uongozi wa shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA, baada ya kuchukizwa na kitendo cha klabu hiyo ya jijini London cha kumrubuni mchezaji wao Neymar da Silva Santos JĂșnior.

Taarifa iliyotolewa jana na uongozi wa klabu hiyo ya nchini Brazil imeeleza kuwa uongozi wa klabu ya Chelsea umethubutu kuvunja sheria za kumsajili mchezaji huyo anaecheza nafasi ya ushambuliaji kwa kufanya nae mazungumzo.

Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kwamba mazungumzo hayo yaliyokwenda kinyume na taratibu, yamefanywa baada ya Ofa ya klabu ya Chelsea kukataliwa na uongozi wa klabu ya Santos ambao ulihitaji kiasi cha Euro million 35 na si Euro million 20 zilizokua tayari kutolewa na The blues.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Santos umesema si klabu ya Chelsea pekee iliyokataliwa kumsajili mchezaji huyo kwa pesa ndogo bali klabu ya, West Ham United, nayo iluituma ofa ya Euro million 15 na kukataliwa lakini wao hawakwenda kinyume na taratibu za usajili zinavyoagiza.

No comments:

Post a Comment