KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 19, 2010

CHELSEA WAJIPANGA UPYA.


Klabu ya Chelsea imeendelea kujizatiti katika utaratibu wa kumsajili mshambuliaji wa pembeni toka nchini Brazil na klabu ya Santos Neymar da Silva Santos Júnior.

Chelsea wameendelea na hatua hiyo baada ya kupandisha dau kutoka paund million 17 hadi 25 ambayo inakaribia dau lililowekwa na uongozi wa klabu ya mchezaji huyo Santos FC la paund million 29.6 kama ada ya uhamisho wake.

Hata hivyo imeelezwa kuwa dili la usajili wa Neymar da Silva Santos Júnior litakamilishwa baada ya mchezaji huyo kuthibitisha safari yake ya kutoka nchini Brazil na kuelekea barani Ulaya ndani ya saa 24 zijazo.

Kabla ya kufanya maamuzi hayo, tayari kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil Mano Menezes amemkanya Neymar da Silva Santos Júnior kwa kumueleza anatakiwa kufikiria mara mbili juu ya safari yake ya Ulaya mbayo hana imani nayo kwani upo uhakika wa kwenda kulikalia benchi hatua ambayo itamuuwia vigumu kumuita katika kikosi cha timu ya taifa hapo baadae.

No comments:

Post a Comment