KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 13, 2010

DILI LA BALOTELLI LAIBUKA TENA.


Baada ya kuwa kimywa kwa siku nne zilizopita wakala wa mshambuliaji kinda wa kimataifa toka nchini Italia pamoja na klabu bingwa barani Ulaya Inter Milan Mario Balotelli ameibuka tena na kusema ana matumaini makubwa mchezaji wake atajiunga na klabu ya Manchester City siku za hivi karibuni.

Mino Raiola wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amesema mazungumzo ya kuuzwa kwa Balotelli huenda yakaendelea tena hii leo lakini usajili wake hautomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza mchezo wa kwanza dhidi ya Tottenham hapo kesho.

Mino Raiola amesema hii leo atajitahidi kwa kila hali kuyafufua mazungumzo yaliyokua yanaendelea na lengo lake kubwa ni kutaka kumuona mchezaji wake anabadili mazingira ya soka lake ambapo toka alipokua mdogo amecheza katika soka la nchini Italia.

Mazungumzo ya Mario Balotelli kujiunga na Man city yalivunjika baada ya mshambuliaji huyo kutaka kulipwa paund 180,000 kwa juma kama mshahara wake wakati uongozi wa klabu ya Man city ulikua tayari kumlipa mshahara wa paund 60,000 kwa juma.

No comments:

Post a Comment