KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 23, 2010

DROO YATOSHA !!!!


Baada ya kulazimisha sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Man utd, meneja wa klabu ya Fulham Mark Hughes amesema kikosi chake kilistahili kusaka matokeo hayo kufuatia ugumu wa mchezo.

Mark Hughes amesema mazingira ya mchezo huo yalikua magumu na kikosi chake kilijikuta kikiwa nyuma kwa idadi ya mabao mawili kwa moja kufuatia Man utd kucheza vyema wakati wote wa mchezo.

Hata hivyo meneja huyo aliejiunga na Fulham kufuatia kuondoka kwa Roy Hodgson alielekea Anfiled, ameongeza kuwa kikosi chake kilionekana kurudi katika mchezo na kufanikiwa kupata matokeo ya sare.

Nae meneja wa klabu ya Man utd Sir Alex Ferguson amesema walistahili kushinda mchezo huo lakini makosa mdogo yaliyojitokeza dakika 10 za mwisho yaliwagharimu kwa kiasi kikubwa.

Amesema kwa ujumla kikosi chake hakikucheza vibaya sana huku akikimwagia sifa kem kem kikosi cha Fulham kwa kuonyesha mchezo wa kutokatishwa tamaa ambao uliwapa upinzani wachezaji wake mpaka dakika ya mwisho.

Nae mfungaji bao la kusawazisha kwa upande wa Fulham Brede Hangeland amesema alistahili kusaka bao hilo kutokana na makosa aliyoyafanya ya kujifunga mwenyewe katika kipindi cha pili na kujikuta akiwazawadiwa Man utd.

Brede Hangeland amesema baada ya kuona nafasi ya kupiga kosa imepatikana dakika 6 kabla ya mchezo kumalizika alijipa matumaini ya kufanya hivyo na akafanikiwa kufuta makosa aliyoyafanya.

Katika mchezo huo mabao ya Man utd yamefungwa na Paul Scholes, na Brede Hangeland aliejifunga mwenyewe na kwa upande wa Fulham Simon Davies akifunga bao la kwanza huku Brede Hangeland akifunga bao la pili.

No comments:

Post a Comment