KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 20, 2010

GALLAS KUICHEZEA SPURS MSIMU HUU.


Aliekua nahodha na beki wa klabu ya Arsenal William Gallas hii leo anatarajia kupimwa afya yake tayari kwa kujiunga na klabu ya Tottenham yenye maskani yake makuu jijini London kwenye uwanja wa White Hart Lane.

Gallas anaratarajia kujiunga na klabu hiyo kwa lengo la kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ambayo imeonekana ikipwaya kufuatia kuumia mara kwa mara kwa Ledley King pamoja na Jonathan Woodgate.

Gallas anatarajia kujiunga na Tottenham, baada ya mkataba wake na klabu ya Arsenal kumalizika msimu uliopita na alipotakiwa kusaini mkatana mwingine alikataa kutokana na matakwa ya viongozi wa klabu hiyo kutaka asaini mkataba wa mwaka mmoja.

Endapo usajili wa beki huyo utakamilika salama, huenda akaanza kuonekana akiwa na klabu hiyo mwishoni mwa juma hili katika michezo ya ligi kuu ya Uingereza pamoja na kati kati ya juma lijalo katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya BSC Young Boys toka nchini Uswiz.

No comments:

Post a Comment