KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 20, 2010

HARYY REDNAPP ATHIBITISHA KUMNASSA GALLAS.


Meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp amethibitisha taarifa za kuwa katika harakati za kumsajili aliekua nahodha na beki wa klabu ya Arsenal William Gallas.

Redknapp amethibitisha taarifa hizo kufuatia taarifa zilizojitokeza kwenye vyombo vya habari mapema hii leo ambazo zimedai beki huyo hii leo alitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya yake kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo ya White Hart Lane.

Meneja huyo amesema ni kweli amevutiwa na beki huyo mwenye umri wa miaka 33, na muda si mrerfu atakua amekamilisha taratibu za kumsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Amesema Gallas, ni mchezaji mzuri na ana uwezo wa kucheza popote pale hivyo ni faraja kwake kumpata beki huyo ambae tayari ameshavichezea vilabu viwili vya jijini London Arsenal pamoja na Chelsea.

Harry Redknapp ameongeza kuwa mbali na Gallas, pia alikua amejipanga kumsajili Joe Cole pamoja na kipa David James kabla ya hawajajiunga na vilabu vilivyowasajili.

Ikumbukwe kuwa William Gallas anatarajia kujiunga na klabu ya Tottenham akiwa kama mchezaji huru, alieondoka Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake kumalizika huko Emirates.


No comments:

Post a Comment