KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 25, 2010

HATUNA HARAKA !!!!!



Bodi ya uongozi wa klabu ya Liverpool imesema hakuna haraka yoyote ya kumuuza kiungo wa kimataifa toka nchini Argentina Javier Mascherano, anaetaka kuondoka huko Anfiled.

Taarifa hizo za bodi ya uongozi zimetoka huku ofa ya klabu ya Barcelona ya paund million 16 ya kutaka kumsajili kiungo huyo ikiwekwa pembeni usiku wa kuamkia jana kabla ya mchezo wa Man city dhidi ya Liverpool waliokubali kisago cha mabao matatu kwa sifuri.

Taarifa hiyo ya Bodi imeendelea kueleza kwamba, klabu ya Liverpool ni kweli inakabiliwa na mzigo wa madeni, lakini haitotumia kigezo hicho kumuuza kirahisi Mascherano.

Liverpool kwa sasa wanadaiwa kiasi cha paund million 350 na benki ya Royal ya nchini Scotland, na ilitegemewa endapo Taykun wa kichina Kenny Huang angefanikiwa kuinunua klabu hiyo deni hilo lingelipwa.

No comments:

Post a Comment