KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 19, 2010

HUGHES AFANYA USAJILI.


Meneja wa klabu ya Fulham Mark Hughes amefanya usajili wake wa kwanza klabuni hapo kwa kumsajili mshambuliaji wa kikmataifa toka nchini Ubelgiji Moussa Dembele.

Fulham wamekamilisha dili la kusajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa ada ya uhamisho wa paund million 5 akitokea kwenye klabu ya AZ Alkmaar ya nchini Uholanzi.

Mark Hughes amezungumza na waandishi wa habari jiji London na kutamba kuwa mshambuliaji huyo atakiongezea nguvu kikosi chake kwa kusaidiana na Bobby Zamora ambae kwa kipindi kirefu alimkosa pacha wake Andy Johnson anaesumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.

Dembele mpaka anaondoka kwenye klabu ya AZ Alkmaar tayari ameshapachika mabao 24 katika michezo 118 ya ligi aliyocheza.

No comments:

Post a Comment