KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 21, 2010

IRELAND AKIWA NA UZI WA ASTON VILLA.Baada ya kukamilisha taratibu zote za kujiunga na klabu ya Aston Villa akitumika kama sehemu ya kubadilishana na Jamaes Milner aliekwenda Man City kiungo wa kimataifa toka nchini Ireland Stephen Ireland amembwatukia meneja wake wa zamani Roberto Mancini kwa kusema si mtu mzuri kwake.

Stephen Ireland amesema kuondoka kwake Man cituy hakukua kwa jambo la kheri bali kumetokana na hali ya kutoelewana na meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italy ambae amedai hana mahusiano mazuri na wachezaji wake.

Amesema mara kadhaa alikua najituma mazoezini kwa mal;engo ya kuilinda nafasi yake katika kikosi cha kwanza, lakini alishangazwa na maamuzi ya meneja huyo kutoa nafasi kwa wachezaji wengine ambao walikua hawana kiwango kama cha kwake.

Amesema ilifikia wakati alikua akimkumbuka Mark Hughes ambae amedai alikua akimpa nafasi kila mchezaji kutokana na mchango wake mazoezini.

Itakumbukwa kuwa kutimuliwa kwa Mark Hughes katika klabu ya Man city mwezi Novemba mwaka jana, kulimpa nafasi meneja waompa nafasi Roberto Mancini kuajiriwa klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment