KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 21, 2010

JOE COLE AKUBALI LAWAMA.


Kiungo mpya wa klabu ya Liverpool Joe Cole amekubali lawama toka kwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya kukosa mkwaju wa penati kwenye mchezo wa hatua ya mtoano uliochezwa juzi kwenye uwanja wa Anfiled dhidi ya klabu ya Trabzonspor toka nchini Uturuki.

Cole amesema suala la yeye kukosa mkwaju wa penati kwake analichukulia kama bahati mbaya lakini kwa upande wa mashabiki hana budi kukubali lawama zinazomuangukia.
Amesema kweli ahatua ya kukosa mkwaju huo iliwavunja nguvu wachezaji wenzake lakini bado anashukuru kwa ushindi wa bao moja kwa sifuri uliopatikana kupitia kwa Ryan Babel katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza.

Katika hatua nyingine kiungo huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza amewataka mashabiki wa Liverpool kusahau yote yaliyopita na kujipanga na mchezo ujao wa ligi ambao utawakutanisha na Man city siku ya jumatatu.

Joe Cole amesema huo ujao dhidi ya Man city utakua mgumu na anaamini wachezaji walisalia kikosini watafanya kazi ya ziada kuhakikisha wanapata ushindi baada ya kuanza kwa matokeo ya sare wakiwa nyumbani msimu huu.

Katika mchezo huo Joe Cole hatojumuishwa kikosini kufuatia kutumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa mwanzo wa ligi kuu walipocheza na Arsenal.

No comments:

Post a Comment