KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 17, 2010

JONES KUJIUNGA NA LIVERPOOL.


Baada ya kujikuta wakipoteza point mbili muhimu katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza mbele ya washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal, majogoo wa jiji Liverpool wamethibitisha kuwa mbioni kukamilisha usajili wa kipa wa klabu ya Middlesbrough Brad Jones kwa uhamisho wa paund million 2.3.

Majogoo wa jiji Liverpool wanatarajiwa kukamilisha usajili huo ambao huenda ukampa changamoto kubwa kipa wao wa sasa Pepe Reina aliefanya makosa makubwa ya kuizawadia bao Arsenal katika dakika za lala salama.

Imesemekana kwamba Jones, mwenye umri wa miaka 28, usiku wa kuamkia hii leo alitarajia kufanyiwa vipimo vya afya yake ikiwa ni sehemu ya hatua za uhamisho kutoka kwenye klabu yake ya sasa na kuelekea Anfiled yalipo makao makuu ya klabu ya Liverpool.

Dili la kipa huyo litakapokamilika Liverpool watakua wamefikisha idadi ya wachezaji sita waliowasajili katika kipindi hiki ambapo miongini mwao yupo Joe Cole, Danny Wilson, Christian Poulsen, Milan Jovanovic and Jonjo Shelvey.

No comments:

Post a Comment