KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 12, 2010

KENWYNE JONES ATIMKIA STOKE CITY.


Huko Britannia Stadium yalipo makao makuu ya klabu ya Stoke City napo kuna taarifa njema kufuatia usiku wa hii leo kukamilika kwa usajili wa mshambuliaji wa kimataifa toka Trinidad and Tobago, Kenwyne Jones.

Stoke City wamekamilisha usajili wa mshambuliaji huyo akitokea Sunderland kwa ada ya uhamisho wa paund million 8 huku wakimsainisha mkataba wa miaka minne.

Meneja wa klabu ya Stoke City Tony Pulis amesema kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo ndani ya kikosi chake, anaamini hatua hiyo italeta changamoto ya ushindani ambayo itamsaidia kupata mafanikio kwenye msimu huu.

Kusajiliwa kwa Kenwyne Jones mwenye umri wa miaka 25, kunamaanisha kwamba ndoto za mshambuliaji wa klabu ya Nice ya nchini Ufaransa Loic Remy kuelekea Britannia stadium katika kipindi hiki zimeyeyuka.

No comments:

Post a Comment