KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 13, 2010

KINDA WA MAN UTD ATIMKIA SUNDERLAND.


Klabu ya Sunderland imeendelea kuweka mkazo katika suala la usajili ambapo usiku wa kuamkia hii leo imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Danny Welbeck kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Manchester United.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19 amejiunga na klabu ya Sunderland baada ya kuitumikia man utd katika michezo 14 ya ligi kuu na kufanikiwa kufunga mabao matano.

Tayari meneja wa klabu ya Sunderland Steve Bruce amesema mshambuliaji huyo atakuwepo kwenye kikosi chake kitakachofungua msimu hapo kesho kwa kucheza na Birmingham City huko Stadium of Light.

Kusajiliwa kwa Danny Welbeck kunamfanya Steve Bruce kuwa na washambulia wanne katika kikosi chake ambao ni Darren Bent, Fraizer Campbell pamoja na Martyn Waghorn.

No comments:

Post a Comment