KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 13, 2010

BECKHAM AMKANA CAPELLO.


Kiungo wa kimataifa toka nchini uingereza David Beckham amesema hayupo tayari kukubaliana na utaratibu wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello wa kumuita kwa mara ya mwisho katika kikosi chake kwa lengo la kuwaaga mashabiki wake.

David Beckham mwenye umri wa miaka 35 amesema kauli ya meneja huyo imemshangaza kwani hakuwahi kumueleza hata siku moja kwamba yu tayari kustahafu soka la kimataifa hivyo kauli hiyo ameitoa yeye binafsi kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza.

Kiungo huyo ambae kwa sasa yupo nchini Marekani akifanya mazoezi ya kumrejesha katika hali yakle ya kawaida baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitano iliyopita amesema yeye binafsi bado anapenda kuichezea timu ya taifa ya Uingereza ambayo amedai kuipenda toka moyoni.

Itakumbukwa kuwa usiku wa kuamkia jana Fabio Capello alivielezwa vyombo vya habari kuwa anatarajia kumuita kiungo huyo kwa mara ya mwisho kwenye kikosi chake ili aweze kuwaaga mashabiki.

Sababu kubwa iliyotolewa na Capello ya kutarajia kufanya hivyo ni kutaka kutoa nafasi kwa vijana kwenye kikosi chake na kuwaacha baadhi ya wachezaji wenye umri mkubwa.

No comments:

Post a Comment