KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 13, 2010

KUMBE INAWAUMA SANAAAAAAAA !


Zikiwa zimesalia saa kadhaa kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza, kiungo mkongwe wa klabu ya Man Utd Ryan Giggs amekiri kuumizwa na kitendo cha ubingwa wa Uingereza kuchukuliwa na klabu ya Chelsea msimu uliopita.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 amesema baada ya kuumizwa na kitendo hicho msimu huu hana namna ya kuwashawishi wachezaji wengine klabuni hapo kucheza kwa kujituma zaidi na kufikia malengo ya kuurejesha ubingwa huko Old Traford ulipodumu kwa misimu mitatu mfululizo.

Amesema haoni sababu ya kushindwa kufikia lengo hilo la kutwaa ubingwa kufuatia kikosi chao msimu huu kuwa na sura mpya ambazo zinaonekana kuwa na uchu wa kuifikisha pazuri Man Utd.

Hata hivyo Giggs amekiri huenda wakakutana na upinzani mkali toka kwa vilabu vingine lakini bado akaendelea kusisitiza kwamba wana kila sababu ya kurejesha heshima yao iliyopotea.

Akimzungumzia Javier Harnandes Chacharito aliesajiliwa toka kwenye klabu ya Deportivo Guadalajara ya nchini Mexico amesema ni mchezaji mzuri na tayari ameshaanza kuonyesha cheche kupitia michezo aliyopewa nafasi kabla ya kuanza kwa msimu sambamba na mchezo wa kuwani ngao ya hisani waliocheza mwishoni mwa juma lililopita na kufanikiwa kuwabamiza Chelsea mabao matatu kwa moja.

Giggs ameongeza kuwa mbali na Javier Harnandes Chacharito pia ana matumaini mshambuliaji wao wa kimataifa toka nchini Uingereza Wayne Rooney ataendelea kuwika kama ilivyokua msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment