KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 17, 2010

MADRID WAMPATA OZIL.


Hatimae meneja wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho amefanikisha azma yake ya kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Ujerumani Mesut Ozil.

Mesut Ozil alietokea kwenye klabu ya Weder Bremen ya nchini ujerumani amejiunga na meneja huyo wa kimataifa toka nchini Ureno baada ya kuhusishwa na taarifa za kuihama klabu yake kwa muda mrefu uliopita.

Miongoni mwa vilabu vilivyokua vinahusishwa na taarifa za kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21, ni pamoja na Chelsea, Arsenal, Man utd zote za nchini Uingereza na FC Barcelona ya nchini Hispania.

Kufuatia kukamilika kwa harakati za usajili wa Ozil kunaifanya klabu ya Real Madrid kuwa na wachezaji wawili wa kijerumani waliowasajili mara baada ya kuwaona kupitia fainali za kombe la dunia zilizomalizika July 11 nchini Afrika kusini.

No comments:

Post a Comment