KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 12, 2010

MAISHA YANGU NI KUHAMA NCHI SI KLABU.


Nahodha na kiungo wa timu ya ta taifa ya Argentina Javie Macherano amesema bado ana matamanio ya kuondoka huko Anfiled yalipo makao makuu ya klabu yake ya Liverpool.

Javie Macherano amesema kutaka kuondoka kwake huko Anfiled hakuhusiani na tatizo lolote ambalo limewahi kujitokea siku za hivi karibuni bali anachotaka ni kubadili mazingira ya soka lake.

Amesema toka aliposajiliwa klabuni hapo mwaka 2007 akitokea West Ham hajawahi kukorofishana na yoyote iwe shabiki, mchezaji mwenzake ama kiongozi hivyo suala la kuhama kwake lisichukuliwe kama ametibuana na baadhi ya watu wa Liverpool.

Akizungumzia suala la kuhusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona na si Inter Milan, kama ilivyokuwa ikizungumzwa siku za nyuma Javie Macherano amesema katika maisha yake hupenda kuhama nchi na sio klabu hivyo suala hilo lisiwashtue mashabiki wake.

Itakumbukwa kuwa kabla ya kuhusishwa na taarifa za kujiunga na klabu ya Barcelona Javie Macherano alikua njiani kumfuta meneja wake wa zamani Rafael Benitez aliepata kibarua huko Inter Milan.

No comments:

Post a Comment