KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 12, 2010

MICHEL BASTOS HAUZWI.


Uongozi wa klabu ya Olympic Lyon ya nchini Ufaransa, umezionya klabu zinazomuwani beki wa kushoto wa klabu hiyo Michel Bastos.

Uongozi wa Olympic Lyon umetoa onyo, huku ukibainisha wazi kwamba katu hautofikiria kumuuza beki huyo wa kushoto toka nchini Brazil katika kipindi hiki kufuatia kuwepo kwenye mipango yao kwa hivi sasa.

Kauli ya onyo imekuja kufuatia klabu za Juventus, Real Madrid pamoja na Arsenal kuwa mstari wa mbele kuwania saini ya mchezaji huyo katika kipindi hiki cha usajili.

Michel Bastos mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na klabu ya Olympic Lyon mwaka 2009 akitokea katika klabu ya Lilley ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa paund million 18.

No comments:

Post a Comment