KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 19, 2010

MILNER AKAMILISHA SAFARI YA MAN CITY.


Hatimae ndoto za klabu ya Man City kumsajili kiungo wa kimatafa toka nchini Uingereza James Milner zimetimia baada ya mchezaji huyo kupimwa afya yake mjini Birmingham hapo jana.

Man City wamemsajili Milner mwenye umri wa miaka 24, kwa mkataba wa miaka mitano, huku wakikubaki kutoa kiasi cha paund million 26 kama ada ya uhamisho wake akitokea Aston Villa.

Mbali na kutoa kiasi hicho cha fedha Man City pia wamekubali kumuachia kiungo wao wa kimataifa toka nchini Ireland Stephen Ireland ambae amejiunga na klabu ya Aston villa.

Meneja wa muda wa klabu ya Aston Villa Kevin MacDonald amesema kuondoka kwa James Milner katika kikosi chake sio pigo kubwa sana baada ya kufanikiwa kumpata Stephen_Ireland ambae ana imani atamsaidia katika harakati za kuwania ushindi kwenye michezo inayomuandama msimu huu.

No comments:

Post a Comment