KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 23, 2010

MNANIONEA BURE JAMANI !!!!!!!!!!


Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini ametetea maamuzi yake ya kutumia fedha nyingi katika usajili wa kikosi chake katika kipindi hiki.

Mancini ametetea maamuzi yake baada ya mameneja wa vilabu kadhaa nchini Uingereza kumlalamikia huku wakidai hatua yake ya usajili huenda ikalifanya soka la nchini humo likawa ghali katika upande wa usajili wa wachezaji.

Mancini amesema kama itakumbukwa vyema vipo vilabu vilishawahi kutumia fedha nyingi katika usajili na si miaka 15 iliyopita bali vimefanya hivyo ndani ya miaka miwili iliyopita hivyo anashangazwa na yeye kulalamikia juu ya usajili anaoufanya.

Utetezi wa Mancini umekuja kufuatia kauli iliyotolewa na meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson akizungumzia hatua ya vilabu kuwania nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu.

Amesema harakati za vilabu kumaliza katika nafasi hizo zimeonekana kuja juu kutokana na baadhi ya wawekezaji kuwekeza fedha nyingi katika usajili.

No comments:

Post a Comment