KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 23, 2010

MWACHENI Shearer AITWE Shearer !!!


Mfungaji wa mabao matatu kati ya sita katika mchezo wa jana wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza kati ya Newcastle Utd dhidi ya Aston Villa Andy Carroll amewataka mashabiki wa The Magpies kutomfananisha na gwiji Alan Shearer.

Carroll, mwenye umri wa miaka 21, ametoa ushauri huo kwa mashabiki wa klabu ya Newcastle baada ya mashabiki hao kuanza kumfananisha na Alan Shearer kufautia uwezo wake mkubwa aliouonyesha katika mchezo wa jana.

Amesema hastahili kufananishwa na mkongwe huyo kutokana na mazuri aliyoyafanya akiwa na klabu hiyo aliyoichezea michezo 303 na kufunga mabao 148.

Andy Carroll ameenedselea kusisitiza kwamba kuvaa jezi nambari 9, nacho kisitumiwe kama kigezo cha kufananishwa na Alan Shearer kwani anaamini jezi na namba ni sehemu ya vazi anapokua mchezoni.

Katika hatua nyingine meneja wa klabu ya Newcastle Utd Chris Hughton amesema mchezaji huyo bado ana nafasi nzuri ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kuitumikia klabu hiyo licha ya kuonyesha makubwa katika mchezo wa jana.

Amesema kutokana na umri wake nafasi hiyo bado anaamini anayo na kama atajituma ipasavyo atakapokuwa uwanjani hakuna litakalo shindikana katika harakati zake za kutaka kujitengenezea historia nzuri ya soka lake akiwa na Newcastle Utd.

No comments:

Post a Comment