KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 18, 2010

NEYMAR KUTOA JIBU LA KUHAMA AMA KUBAKI.


Uongozi wa klabu ya Chelsea upo katika hatua ya kusubiri harakati za kumsajili winga wa kimataifa toka nchini Brazil pamoja na klabu ya Santos Neymar da Silva Santos Júnior.

Chelsea wanasubiri kukamilisha hatua hiyo kufuatia winga huyo kupewa muda wa kutoa msimamo wake wa kuendelea kubaki nchini Brazil ama kuondoka na kuelekea barani laya.

Mwenyekiti wa klabu ya Chelsea Bruce Buck amethibitisha huenda juma hili wakamsajili Neymar da Silva Santos Júnior endapo mchezaji huyo atatoa maamuzi ya kuondoka nchini Brazil na kuachana na klabu yake ya Santos.

Hata hivyo taarifa zimeeleza kwamba usajili wa Neymar da Silva Santos Júnior mwenye umri wa miaka, 18 huenda akazua gumzo kutokana na Chelsea kutayarisha kiasi cha paund million 24 kama ada ya uhamisho huku uongozi wa klabu ya Santos ukiripotiwa kutaka kiasi cha paund million 29.6.

Wakala wa Neymar, Wagner Ribiero amesema kabla ya mchezaji wake hajatoa msimamo wa kubaki nchini Brazil ama kuondoka, atakutana na familia yake katika kikao maalum ambacho kitaamua nini afanye katika maamuzi yake.

No comments:

Post a Comment