KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 23, 2010

NI BONGE LA KIPA.


Nae meneja wa klabu ya Bolton Wanderers Owen Coyle ameshindwa kujizuia na kujikuta akimsifia kipa wake nambari moja Jussi Jaaskelainen kufuatia kuonyesha mchezo mzuri katika pambano la mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya West Ham UTD.

Owen Coyle amesema kwa kiasi kikubwa kipa huyo alichangia kuisaidia Bolton kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja mbele ya West Ham Utd ambao walikua nyumbani huko Upton Park.

Amesema ujasiri wa kipa huyo wa kimataifa toka nchini Finland na hatua za kujituma kwake kila mara, kuliwapa wakati mgumu wachezaji wa West Ham Utd na kubwa zaidi ni pale alipookoa penati iliyopigwa na Carlton Cole's katika kipindi cha kwanza.

Katika mchezo huo mabao mabao aya Bolton Wanderers yalikwamishwa kimiani na Mathew Upson aliejifunga mwenyewe katika dakika ya 48 pamoja na mshambliaji wa kimataifa toka nchini Sweden Johan Erik Calvin Elmander huku bao la West ham utd likifungwa na Mark Noble katika daika ya 79.

No comments:

Post a Comment