KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 18, 2010

NILITAMANI KUCHEZA HADI KUFA.


Siku moja baada ya shirikisho la soka nchini ufaransa kutangaza adhabu kwa baadhi ya wachezaji waliokua na timu ya taifa ya nchi hiyo huko Afrika kusini kwenye fainali za kombe la dunia, mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Nicolus Anelka ambae ni muhanga wa adhabu hiyo amezungumzia suala hilo.

Anelka amesema adhabu iliyotolewa na shirikisho la soka nchini kwao Ufaransa katu haimuingii akilini na kwake anaiona kama inamnyima nafasi kocha wa sasa Laurent Blanc kufanya kazi yake kwa amani.

Amesema aliposikia adhabu yake ya kufungiwa michezo 18 ya timu ya taifa alijisikia kucheka hadi kufa kutokana na adhabu hiyo kutokua na uzito wa kosa lililojitokeza nchini Afrika Kusini walipokua kwenye fainali za kombe la dunia.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31,ameongeza kwamba suala la adhabu dhidi yake limeshafikia hatamu toka alipoaondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa mnamo June 19 mwaka huu.

Mbali na Anelka kupewa adhabu ya kutokucheza michezo 18 ya timu ya taifa, aliekua nahodha wa kikosi cha Ufaransa katika fainali za kombe la dunia Patrice Evra, nae ameadhibiwa kutokucheza michezo mitano, Frank Ribery adhabu yake ni kutokucheza michezo miwili, na Jérémy Toulalan amefungiwa mchezo mmoja huku Erick Abidal akiepuka adhabu hizo baada ya utetezi wake kukiridhisha kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho la soka nchini Ufaransa.

No comments:

Post a Comment