KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 19, 2010

NIMEKUJA KUSHINDA MATAJI.


Kiungo wa pembeni James Milner aliekamilisha dili la kujiunga na klabu ya Man City usiku wa kuamkia hii leo, ametambulishwa kwa mashabiki wa klabu hiyo na kukabidhiwa jezi namba saba.

James Milner ametambulishwa rasmi baada ya kusajiliwa kwa dali la uhamisho wa paund million 24 akitokea kwenye klabu ya Aston villa ambayo pia imefaidika kumsajili aliekua kiungo wa Man City Stephen Ireland.

Baada ya kuabidhiwa jezi namba saba na kutambulishwa kwa mashabiki, James Milner alipata nafasi ya kuzungumza na kudai kwamba amejiunga na klabu hiyo kwa lengo la kutwaa ubingwa wa michuano mbali mbali wanayoshiriki msimu huu.

Amesema kwa uwezo wake binafsi pamoja na ushrikiano utakaokuwepo kutoka kwa wachezaji wengine wa klabu hiyo, kutaiwezesha Man city kufikia malengo yaliyowekwa katika kipindi hiki cha msimu wa mwaka 2010-11.

Kusajiliwa kwa James Milner kuinaifanya klabu ya Man City kufikisha idadi ya wacdhzaji 7 waliowasajili katika kipindi hiki ambao ni Mario Balotelli, Jerome Boateng, Alex Henshall, Aleksandar Kolarov, James Milner, Yaya Toure pamoja na David Silva.

No comments:

Post a Comment