KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 14, 2010

REDNAPP AMPA 5 JOE.


Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspours Harry Rednapp amempa tano kipa wa klabu ya Man city Joe Hart kwa uwezo mkubwa aliouonyesha katika mchezo wa ufunguzi wa ligi uliozikutanisha klabu hizo mbili hii leo alasiri.

Rednapp amesema kipa huyo amekua muhimili mkubwa katika mchezo wa hii leo kwa kwa asilimia kubwa ameuokoa upande wa man city ambao ulikua na kila sababu za kupoteza mchezo wa hii leo.

Amesema kasi iliyoonyesha na wachezaji wake katika kipindi cha kwanza ulikua inampa hamasa ya kuhisi huenda wangepata bao la kuongoza lakini kwa umahiri wa kipa huyo wachezaji wake alishindwa kukamiolisha lengo hilo.

Nae meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini amba amekaukwa na sauti kufuatia kufanya kazi ya kuwapigia kelele wachezaji wake ambao amekiri walizidiwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Alipoulizwa juu ya uchaguzi wa kipa, Mancioni aligoma kulizungumzia suala hilo hukua kisema bado ni mwenye furaha kwa kuwa na makipa wawili wenye uwezo mkubwa ambao amedai wanampa nafasi ya kufanya maamuzi ya nani atacheza katika mchezo gani.

No comments:

Post a Comment