KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 20, 2010

ROBINHO KUUZWA WIKI IJAYO.


Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini amesema huenda akamuuza mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Brazil Róbson de Souza Robinho ndani ya siku tano ama sita zijazo.

Roberto Mancini amesema anatarajia kufanya hivyo kufuatia mchezaji huyo kuwa tayari kuondoka klabuni hapo baada ya kumpeleka kwa mkopo kwenye klabu ya Santos nchini kwao Brazil mwanzoni mwa mwaka huu.

Amesema toka mchezaji huyo alipowasili huko Eastland siku nne zilizopita amekua akiushawishi uongozi umruhusu kuondoka na kujiunga na klabu moja wapo ya huko nchini Uturuki.

Mbali na suala la Robinho, Mancini pia amezungumzia mustakabali wa kipa Shay Given pamoja na mshambuliaji Roque Santa Cruz kwa kusema suala la wachezaji hao nalo litapatiwa ufumbuzi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwishoni mwa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment