KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 25, 2010

SAFARI YA LONDON YAZUA JAMBO.


Meneja wa klabu ya Stoke City Tony Pulis amemkalipia wazi wazi kipa wake chaguo la pili Asmir Begovic baada ya kugoma kucheza mchezo wa jana wa michuano ya kombe la ligi dhidi ya klabu ya Shrewsbury Town.

Tony Pulis amesema alipanga kumtumia kipa huyo katika mchezo huo wa ligi uliomalizika kwa kikosi chake kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja lakini mapema jana asubuhi kipa huyo alimueleza hayupo tayari kucheza hatua ambayo ilimlazimu kumtumia kipa wake nambari tatu Carlo Nash huku akimuweka benchi kipa wake namba moja Thomas Sorensen .

Hata hivyo inadhaniwa huenda hatua ya kugomea mchezo wa jana kwa Asmir Begovic raia toka nchini Bosnian imetokana na uongozi wa klabu ya Stoke city kugoma kusikiliza ofa ya klabu ya Chelsea iliyoonyesha nia ya kutaka kumsajili katika kipindi hiki.

No comments:

Post a Comment