KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 23, 2010

SASA FA WANATAKIWA KUBADILIKA !!!


Baada ya muamuzi Chris Foy kukataa bao la klabu ya Stoke City mwishoni mwa juma lililopita kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya klabu ya Tottenham meneja wa The Potters Tony Pulis ameutaka uongozi wa chama cha soka nchini humo kutazama upya sheria ya kutumika kwa teknologia ya televisheni.

Tony Pulis amesema kitendo cha muamuzi Chris Foy kulikataa bao lao ambalo lingewapa matokeo ya sare katika mchezo huo uliomalizika kwa kufungwa mabao mawili kwa moja, kuna maanisha muamuzi huyo hakuona nini kilichotolea langoni mwa Spurs.

Amesema kutokaana hali hiyo ipo haja ya uongozi wa chama cha soka nchini Uingereza kuidhinisha hatua ya kutumika kwa teknologioa hiyo ambayo anaamini itamaliza utata wa mabao yatakayofungwa katika ligi msimu huu pamoja na kwenye michuano mingine.

Hata hivyo ombi hilo la meneja wa klabu ya Stoke City limeonekana kuungwa mkono na muamuzi wa zamani wa nchini Uingereza Dammy Galler alipokua akizungumzia utata wa bao uliojitokeza katika mchezo huo.

Dammy Galler amesema chama cha soka nchini Uingereza kinastahili kutumia teknologia hiyo ya televisheni lakini si katika mchezo wote wa soka bali inatakiwa kutumika katika hatua ya kuthibitisha ukweli wa kitendo kitakachozua utata.


Wakati huo huo meneja wa klabu ya Stoke city Tony Pulis ametangaza kutokuwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Tottenham Peter Crouch.

Pulis amesema anaamini mchezaji huyo bado ni mwenye furaha huko White Hert Lane hivyo ni vigumu kwake yeye kumsajili katika kipindi hiki ambacho anaamini Spurs wanaendelea kujijenga.

Amesema mchezaji anae muwania kwa sasa ni mshambuliaji wa klabu ya Cardiff Jay Bothroyd ambae anaamini ataziba mwanya ulioachwa na Mamady Sidibe alie majeruhi.

No comments:

Post a Comment