KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 17, 2010

SCHOLES AMKUNA BABU.

Baada ya ushindi wa mabao matatu kwa sifuri uliopatikana usiku wa kumakia hii leo mbele ya Newcastle UTD, meneja wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amemwagia sifa kede kede kiungo wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Paul Scholes.

Sir Alex Ferguson amemsifia kiungo huyo kwa kusema yeye ndie chachu ya ushindi wao wa kwanza walioupata katika msimu huu wa ligi kwa kuibamiza Newcastle Utd ambayo iliwapa upinzani wa kutosha.

Mzee huyo toka nchini Scotland amesema anaamini kiwango alichokionyesha Scholes katika mchezo wa jana bado kitaendelea kutoa hamasa katika utafutaji wa ushindi kwenye michezo mingine ya ligi.

Katika mchezo huo Man Utd walikua nyumbani old Trafford na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri yaliyofungwa na Dimiter Berbatov 33’ Daren Fletcher 42 pamoja na Ryan Giggs 85.

No comments:

Post a Comment