KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 25, 2010

SIHUSIKI HATA KIDOGO !!!!!!


Winga wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Man City James Milner amesema hastahili kuhusishwa na hatua ya kuondoka kwa aliekua meneja wa klabu ya Aston Villa Martin O’Neil.

Milner amelazimika kuutaka umma wa mashabiki wa soka ulimwenguni kote kutomuingiza katika tanuri hilo huku akidai uhamisho wake haukua chanzo cha kuondoka kwa meneja huyo wa kimataifa toka Ireland Kaskazini.

Amesema uhamisho wake ulianza kusikika kupitia vyombo vya habari toka mwishoni mwa msimu uliopita hivyo ni ujinga hii leo maneno kuibuka na kudai uhamisho wake umesababisha.

Milner alieihama Aston villa juma lililopita ameongeza kwamba hatua ya kuondoka kwa Martin O’Neil anatakiwa kuulizwa yeye mwenyewe na ana imani atatoa majibu yaliyo sahihi.

No comments:

Post a Comment