KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 24, 2010

SIJAFUNGA MIMI KAFUNGA MSHAMBULIAJI.


Beki wa klabu ya Man City Micah Lincoln Richards amemaliza mzizi wa fitna miongoni mwa waandishi wa habari za michezo toka nchini Uingereza kufuatia bao la pili la klabu hiyo katika mchezo wa jana dhidi ya Liverpool.

Micah Lincoln Richards amemaliza mzizi huo wa fitna kufuatua utata kuzuka miongoni mwa waandihi hao ambao walikua wakijiuliza ni nani mfungaji wa bao hilo, ambapo miongoni mwao walisikika wakisema mpira wa kichwa uliopigwa na beki huyo haukuguswa na Carlos Teves kabla haujaingia ndani ya kimia.

Alipohijiwa beki huyo mwenye umri wa miaka 22 alisema bao la pili limefungwa na Carlos Teves huku akitoa sababu kwamba mchezaji huyo ni mshambuliaji hivyo kazi yake ni kufunga mabao.

Micah Lincoln Richards pia ameonyesha kufurahishwa na usajili uliofanywa klabuni hapo kwa kusema wachezaji waliosajiliwa wameonyesha uwezo mkubwa wa kukisaidia kikosi cha Man City kupata ushindi wao wa kwanza wa ligi msimu huu mbele ya Liverpool.

Katika mchezo huo wa jana Man City walifanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri yaliyofungwa na Gareth Barry 13 pamoja na Carlos Tévez 52 na 67.

No comments:

Post a Comment