KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 19, 2010

SIKUGOMBANA NA MANCINI- BELLAMY


winga wa kimataifa toka nchini Wales Craige Bellamy ameendelea kukanusha taarifa za kuondoka kwa ugomvi huko Eastland yalipo makao makuu ya klabu ya Man City ambapo safari hii akimzungumzia meneja wa klabu hiyo Roberto Mancini.

Craige Bellamy amesema meneja huyo ni mtu mzuri na katu hakuwahi kugombana nae lakini hakupendezewa na taratibu zake za kutokuzungumza nae juu ya mustakabali wake kwa muda wa miezi sita iliyopita.

Hata hivyo Bellamy amemtakia kila la kheri Mancini katika harakati zake za kusaka ubingwa na kwa upande wake anajisikia ni mwenye furaha kiakili hadi kimwili baada ya kuanza maisha mapya akiwa na klabu ya Cardiff City.

Katika hatua nyingine amesema kwa sasa anajipanga kuisaidia klabu ya nyumbani kwao ili iweze kucheza ligi kuu ya Uingereza msimu ujao licha ya kutambua mwanzo utakua mgumu kuzoea mazingira ya ligi daraja la kwanza.



No comments:

Post a Comment