KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 14, 2010

SIONDOKI CHELSEA NG'O !!!!Kipa tegemezi katika kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Chelsea Petr Cech amekanusha uvumi unaomuandama wa kutaka kujiunga na meneja wake wa zamani Jose Mourinho huko Real Madrid.

Cech amesema taarifa hizo katu hakuwazi kuzizungumza katika chombo chochote cha habari na katu hatofikiria suala la kuihama klabu ya Chelsea iliyomsajili mwaka 2004 akitokea Stade Rennais ya nchini ufaransa.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 28, ameendelea kusistiza kwamba bado anauheshimu mkataba wake na klabu ya Chelsea na atajiona punguwani endapo ataondoka klabuni hapo ambapo amedai anatimiziwa kina nachokitaji.

Amesema wapo baadhi ya wachezaji waliokua tayari kujiunga na Mourinho huko St bernabeu na wamefannikiwa huku akimtolea mfanobeki wa kimataifa toka nchini Ureno Ricardo Carvalho aliekamilisha dili hilo kwa ada ya paund million 6.7 siku tatu zilizopita.

Wakati huo huo, meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti amejiondoa katika kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa kimataifa toka nchini Brazil na klabu ya Benfica David Luiz Moreira Marinho.

Carlo Ancelotti aliingia katika vita ya kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 23, baada ya kufanikisha utaratibu wa kumuuza beki wa Ricardo Carvalho aliejiunga na klabu ya Real Madrid.

Hata hivyo amesema baada ya kujiondoa katika utaratibu wa kumsajili David Luiz, Carlo Anceloti ametangaza kumtumia beki kinda toka katika kikosi chake cha pili Jeffrey Bruma .

No comments:

Post a Comment