KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 20, 2010

SIONDOKI WEST HAM UTD - COLE.


Hatimae Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya West Ham Utd Carlton Cole ametoa msimamo wake na kusema hategemei kuachana na klabu hiyo kwa sasa licha ya klabu kadhaa kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Carlton Cole amesema matarajio yake ya kutaka kuendelea kubaki klabuni hapo ni kufuatia furaha aliyonayo inayotokana na maisha mazuri anayoishi na wachezaji, viongozi pamoja na mashabiki.

Amesema lengo lake ni kuhakikisha anakua klabu hapo kwa kipindi kirefu na ikiwezekana maisha yake yote ya soka ayamalizie hapo hivyo ni vigumu kuondoka.

Ikumbukwe kuwa Carlton Cole mwenye umri wa miaka 26 kabla hajajiunga na West Ham Utd alikua mchezaji wa klabu ya Chelsea ambapo akiwa huko alipelekwa kwa mkopo katika klabu za Wolves, Charlton Athletic na Aston Villa kabla ya kuuzwa moja kwa moja huko Upton Park.

No comments:

Post a Comment