KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Sunday, August 22, 2010

SIRI YAFICHUKA.


Kipa nambari moja katika kikosi cha timu ya taifa ya Italia Gianluigi "Gigi" Buffon amepasua ukweli wa kukataa kujiunga na klabu ya Man City ya nchini Uingereza iliyokua tayari kumsajili katika kipindi hiki.

Gianluigi "Gigi" Buffon amesema sababu kubwa iliyomfanya kukataa ofa hiyo ni kufuatia safu mbovu ya ulinzi ya klabu hiyo iliyojipanga kufanya maajabu msimu huu kwa kumaliza na taji la michuano yoyote wanayoshiriki.

Amesema alitambua kama angejiunga na klabu hiyo inayomilikiwa na kibopa wa kiarabu Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan kazi ingekua kwake na huenda angejishushia hadhi ya umakini anapokua uwanjani.

Hata hivyo kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 amesema bado anaamini marafiki zake wa karibu pamoja na mashabiki wa soka ulimwenguni kote huenda walishangazwa na kitendo hicho cha kukataa kujiunga na klabu hiyo tajiri, lakini akaendelea kushikilia msimamo wake wa kudai safu mbovu ya klabu hiyo ndio chanzo.

Katika hatua nyingine Gianluigi "Gigi" Buffon ametoa ushauri wa bure kwa meneja wa kikosi hicho Roberto Mancini kulizingatia suala hilo la ubovu wa safu yake ya ulinzi na kama atashindwa kulifanyia kazi huenda akashindwa kutimiza ndoto zake za kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Kwa sasa kikosi cha Man City kina mabeki 11 kutoka nchi mbali mbali ambao ni Micah Richards, Wayne Bridge, Joleon Lescott, Shaleum Logan, Javan Vidal, (Uingereza) Pablo Zabaleta (Argentina), Aleksandar Kolarov (Serbia), Jérôme Boateng (Ujerumani), Greg Cunningham(Jam Ireland), Kolo Touré (Ivory Coast), Dedryck Boyata (Ubelgiji).

No comments:

Post a Comment