Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa mwaka 2010-11 hatua ya mtoano imendeelea tena usiklua wa kuamkia hii leo kwa michezo kadhaa kuchezwa katika viwanja tofauti.
Katika uwanja wa Wankdorf wenyeji BSC Young Boys wameanza vyema katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano baada ya kuibanjua Tottenham Hotspours mabao matatu kwa mawili.
Mabao ya BSC Young Boys katika mchezo huo yamefungwa na Senad Lulic 4, Henri Bienvenu 13, na Xavier Hochstrass 28 huku mabao ya Tottenham ya kufutia machozi yakifungwa na Sebastian Bassong 42 na Roman Pavlyuchenko 83.
Meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp amesema licha ya kupokea kichapo cha mabao matatu kwa mawili bado kwake ni faida kubwa katika mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini London juma lijalo.
Rednapp amesema tofauti ya bao moja iliopo katika idadi ya mabao waliyofungwa bado anaamini wataifikia na kufanikisha safari ya kusonga mbele.
Michezo mingine ya michuano hiyo iliyochezwa jana ni pamoja na
Petrovski Stadium (20,000)
Zenit St Petersburg 1 - 0 AJ Auxerre
Valeri Lobanovski (16,000)
Dynamo Kiev 1 - 1 Ajax Amsterdam
Lerkendal (18,800)
Rosenborg 2 - 1 FC Copenhagen
AXA Arena (19,000)
Sparta Prague 0 - 2 MSK Zilina
Michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani ulaya iliyo kwenye hatua ya mtoano inaendelea tena hii leo huko
Estadio Municipal de Braga
Braga v Sevilla FC
St Jakob Park
FC Basel v Sheriff Tiraspol
FK Partizan Stadium
Partizan Belgrade v Anderlecht
Bullen-Arena
SV Salzburg v Hapoel Tel-Aviv
Weserstadion
Werder Bremen v Sampdoria
No comments:
Post a Comment