KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 12, 2010

THE STORY OF BECKHAM IS OVER !!!!


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amesema atamuita kwa mara ya mwisho kiungo wa klabu ya LA Galax ya nchini Marekani David Beckham katika kikosi chake kwa lengo la kuwaaga mashabiki wake.

Fabio Capello ameliweka hadharani jambo hilo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kujipima ubavu dhidi ya timu ya taifa ya Hungary ambao ulimalizika kwa Uingereza kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja, mabao yaliyofungwa na Steven Gerrard katika dakika 70 na 73 huku Philly Jagielka akiizawadia bao Hungary katika dakika ya 62.

Amesema lengo kumpa nafasi ya mwisho kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35 ni kutaka kutoa nafasi kwa vijana chipukizi katika kikosi chake ambacho kinakabiliwa na michezo ya kuwani nafasi ya kushiriki fainali za mataifa ya ulaya mwaka 2010.

Dauid Beckham, mpaka sasa ameshaicheza timu ya taifa ya Uingereza michezo 115 na kwa mara ya kwanza aliichezea timu hiyo mwezi September mwaka 1996 dhidi ya timu ya taifa ya Moldova.

No comments:

Post a Comment